Kaimu Mkuu wa polisi Kenya ahukumiwa miezi 6 jela
13 Septemba 2024Matangazo
Kortini ilimtaka afisa huyo kutoa maelezo kuhusu wapi waliko wanaume watatu wanaodaiwa kutekwa nyara na maafisa wa polisi.
Jaji katika kesi hiyo alikuwa ameahirisha kutoa uamuzi kwa siku saba ili kumpa Masengeli nafasi ya mwisho kufika kortini kabla ya hukumu kutolewa.
Soma pia:Vyombo vya usalama vya Tanzania vyalaumiwa kwa mauaji
Hukumu hiyo inatokana na kesi iliyowasilishwa na Chama cha Wanasheria wa Kenya kutaka mahakama itoe agizo la kuachiliwa na kufikishwa mahakamani watu watatu waliokamatwa na polisi mwezi Agosti na hadi sasa hawajaonekana wala kusikika.