Mkuu wa Shirika la IAEA kuizuru Iran hivi karibuni
10 Novemba 2024Safari hiyo aliyosema itafanyika siku chache zijazo inatarajiwa, wakati kukiwa na mivutano mikali Mashariki ya Kati kutokana na vita kati ya Israel na kundi la Hamas. Itafanyika pia kukiwa na hali ya sintofahamu baada ya Donald Trump kushinda urais katika uchaguzi wa Marekani.
Soma zaidi: IAEA ina wasiwasi kuhusu vinu vya nyuklia vya Iran
Katika ziara hiyo Grossi atafanya mikutano ya ngazi ya juu na serikali ya Iran na atafanya mijadala ya kiufundi katika vipengele vyote vinavyohusiana na kauli ya Pamoja iliyokubaliwa na Iran Machi 2023.
Ziara ya Grossi inakusudiwa kutoa mwelekeao kwa ushirikiano kati ya shirika la kudhibiti nishati ya nyuklia la IAEA na Iran kuhusu kutanua ukaguzi katika mradi wa silaha za atomiki unaozidi kukua nchini humo. Iran inaendeleza mradi huo na inaendelea kuongeza shehena ya Urani iliyorutubishwa na kufikia viwango vya silaha na kukiuka matakwa ya kimataifa, kwa mujibu wa IAEA.