1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiIndia

Modi aapa kuifanya India kuwa kitovu cha uzalishaji duniani

14 Aprili 2024

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ameapa kuongeza matumizi ya kijamii, kuimarisha miundombinu na kuifanya India kuwa mzalishaji mkuu wa kimataifa.

https://p.dw.com/p/4eju0
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akitangaza sera zake wakati wa kampeni ya uchaguzi huko Meerut India: 31.03.2024Picha: Altaf Qadri/AP Photo/picture alliance

Kiongozi huyo analenga kuchukua hatua hiyo wakati makampuni yakiachana na China. Modi amesema hayo wakati akizindua mkakati wa chama chake kuelekea uchaguzi.

Modi ameahidi kutanua mipango ya kijamii iliyoanzishwa na chama chake kinachotawala kwa miaka kumi sasa, ambazo ni pamoja na mamilioni ya nyumba kwa ajili ya watu masikini pamoja na huduma za afya, gesi ya kupikia na mbegu za bure.

Serikali yake imekuwa ikiwalipa wakulima masikini dola 63 kwa mwaka. Amesema sera za serikali yake zimewasaidia watu milioni 250 kuondokana na umasikini tangu alipoingia madarakani mwaka 2014.

Modi, anawania kurejea tena kwa awamu ya tatu. Na yeye pamoja na viongozi wengine wa chama cha Bharatiya Janata wamezindua ahadi hizo kabla ya kuanza kwa uchaguzi mkubwa kabisa nchini humo.