MOGADISHU : Waislamu wadhibiti kitongoji muhimu
2 Desemba 2006Vuguvugu la Kiislam lenye nguvu leo hii limedhibiti kitongoji muhimu cha Somali na kuipeleka nchi hiyo karibu na ukingo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Wakati jumuiya ya kimataifa ikiwa mbioni kuepusha mapambano mapya vikosi vya muungano wa mahkama za Kiislam wamesema wamechukuwa udhibiti wa Dinsoor kitongoji kilioko kama kilomita 270 magharibi mwa mji mkuu wa Mogadishu baada ya wanamgambo wanaoiunga mkono serikali kujiondowa kwenye kitongoji hicho.
Kutwaliwa kwa mji huo ambako kunakiuka makubaliano ya suluhu ya kusitisha mapigano na kutambuana kati ya Muungano wa Mahkama za Kiislam na serikali ya mpito nchini Somali kunakuja siki kadhaa baada ya bunge la Ethiopia kuidhinisha mipango ya Waziri Mkuu Meles Zenawi kupambana na uongozi huo wa Kiislam nchini Somali.