Moldova yapiga kura kuhusu mustakabali wa Umoja wa Ulaya
3 Novemba 2024Hapo awali ya kura ya maoni ambayo ilionyesha ushindi wa asilimia 50.35 kwa upande unaopendelea Umoja wa Ulaya.
Rais wa sasa, Maia Sandu, alipata asilimia 42.5 katika duru ya kwanza, huku Alexandr Stoianoglo, anayeungwa mkono na Urusi, akipata asilimia 26.
Sandu alilaumu uingiliaji wa kigeni kwa matokeo finyu ya kura ya maoni na alidai polisi iligundua mpango wa Urusi wa kununua kura. Katika siku ya uchaguzi, alisisitiza umoja ili kulinda uhuru na kuonya dhidi ya kununua kura.
Soma pia:Moldova yaridhia kwa wingi mdogo kujiunga na EU
Mamlaka ziliripoti ongezeko la vitisho kwa wapiga kura, huku Waziri Mkuu Dorin Recean akisema hali hiyo ni jaribio la kuleta hofu.
Ingawa wagombea wote wanadai kuunga mkono EU, Stoianoglo, ambaye alikataa kura ya maoni, anapigia upatu sera ya usawa katika siasa za kigeni, jambo ambalo linaweza kukwamisha malengo ya Moldova kujiunga na Umoja wa Ulaya iwapo atashinda.