Serikali ya Kenya ilizindua mpango wa kununua mifugo kutoka kwa wafugaji kama njia ya kuwasaidia kukabiliana na hali ya kiangazi inayoshuhudiwa kwa sasa nchini humo, huku makundi mengine ya watu katika jamii yakionekana kama yameachwa kando. Sudi Mnette amezungumza na Naibu Gavana wa Jimbo la Marsabit, Solon Riwe, kuhusu mpango huo. Ameanza kwa kueleza namna watakavyofaidika na mpango huo.