Rais Uhuru Kenyatta anakabiliwa na upinzani mpya kuhusu mpango wa kuwapatanisha Wakenya maarufu BBI katika ngome yake ya siasa ya Mlima Kenya. Wakati huo huo, makundi ya kutetea haki za binadamu yanaitaka serikali kuweka mipango ya kutoa hamasisho kwa Wakenya kabla ya kufanyika kwa marekebisho ya katiba.