1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mratibu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa atembelea Beirut.

23 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG4o

Mratibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya misaada ya dharura, Jan Egeland, amekuwa akitembelea maeneo yalioharibiwa katika viunga vya kusini mwa Beirut huko Lebanon. Alisema nguvu nyingi zilitumiwa katika maeneo yanayokaliwa na raia wengi. Alisema jambo hilo ni kwenda kinyume na sheria za kimataifa. Bwana Egeland pia alizilaumu pande zote mbili kwa mchango wao katika kile alichokielezea kuwa ni vita visivotumia akili. Alisema idadi ya watu waliopoteza makaazi yao huko Lebanon itaongezeka sana. Zaidi ya watu 500,000 wameshalazimika kuyahama majumba yao. Bwana Egeland ameitaka Israel ifanye zaidi kuruhusu misaada ya dharura iwafikie raia wa Lebanon.