Mripuko wa gruneti waua watu 2 Bujumbura
11 Mei 2020Ni mripuko mkubwa ulosikika hadi masafa ya mbali ya jiji la Bujumbura kwenye majira ya saa moja unusu usiku wa kuamkia leo. Mgahawa unaotambulika kama KwaPatrick, mfwasi wa chama Cndd Fdd kwenye barabara ya 11 katika mtaa wa kamenge ndio ulokuwa umelengwa.
Wakaazi wa maeneo ya kando kando na eneo la tukio wanasema mripuko wa guruneti hiyo uliwafanya kupagawa na kuona moshi mkubwa ukipanda juu huku watu kadhaa waliojeruhiwa wakipiga kelele.
"Niliona watu wamekufaa wakiwa chini, wengine wakiwa na majeraha huku wakipiga kelele. Huku wengine wakiwekwa kwenye gari na kupelekwa
hospitali. Nilipatwa na hofu na kulazimika kuondoka eneo hilo ili nisije kukamatwa". Amesema mtu mmoja aliyeshuhudia.
Taarifa zinasema mtu mwingine wa 3 amefariki akiwa hospitali aliko kuwa akipata matibabu. Shambulio hilo limetokea wakati raia mwingine mmoja alotajwa kuwa mfuasi wa chama cha upinzani CNL aliuwawa na wengine 8 kujeruhiwa katika tarafa ya Kiremba mkoa Ngozi, katika makabiliano na baadhi ya vijana wafuasi wa chama tawala. Picha zilotanda kwenye mitandao ya kijamii zikionesha majeruhi walokatwa kwa mapanga.
Hali hiyo ni wakati kumekuwa kukisikia kauli za vitisho kutoka kwa baadhi ya maafisaa. Steve Habimana mmoja ya washauri wa Rais Nkurunziza ameseikika akisema endapo kutakuwepo na watakao pinga matokeo ya uchaguzi basi watakiona cha mtema kuni. Na kwamba Agathon Rwasa hatopata fursa ya kukimbia nchi, kwani hii si 1993 wala 2015. Kwani sasa jeshi na polisi viko imara.
Rais wa zamani Sylvestre Ntibatunganya amewasihi wagombea na wanasiasa kwa jumla kuepuka kauli zinazo zusha uhasama.
Hayo yanajiri wakati Waangalizi wa uchaguzi kutoka jumuia ya Afrika Mashariki EAC huenda wasishiriki katika uchaguzi huo wa mei 20, ambapo
zimesalia siku 9 kabla ya uchaguzi huo huku tume CENI ikimawataka endapo wataingia Burundi kufikia kwanza Karantini kwa siku 14.