Mripuko wauwa polisi 11 Uturuki
26 Agosti 2016Kituo cha televisheni cha NTV nchini humo kimeonyesha moshi mzito ukifuka kutoka katika eneo la tukio,ambacho kimesema ni eneo la ukaguzi la polisi. Cizer ni eneo la mpakani lililopo eneo la jimbo la Sirnak ambalo linapakana na matiafa ya Syria na Iraq. Eneo hilo lina idadi kubwa ya watu wa jamii ya Kikurdi.
Picha za kituo hicho cha televisheni lilionesha uharibufu mkubwa wa ofisi la jengo hilo, huku ikinukuliwa wizara ya afya ikisema imetuma magari ya wagonjwa kwenda katika eneo hilo.
Hali katika hopitali
Na vyanzo vingine kutoka hospitali vikisema takribani idadi hiyo ya watu tisa imeuwawa na wengine 64 wamejeruhiwa. Shirika la habari la taifa Anadolu limetupa lawama ya shambilizi hilo kwa wapiganaji wa chama cha wafanyakazi wa kikurdi PKK ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara tangu makubaliano ya kuweka chini silaha baina yake na serikali kuvunjika mwezi Julai.
Katika tukio lingine lililotokea Alhamis jioni, jeshi la Uturuki lilishambulia eneo la ngome ya waasi la kaskazini mwa Syria. Mapema leo shirika la habari la Anadolu limesema hatua hiyo ilitekelezwa baada ya waasi kukaidi matakwa ya kuwataka waondoke eneo la mashariki.
Jeshi la Uturuki lilivurumisha makombora yake katika kikosi kiitwacho " People's Protection Units (YPG), tawi la kijeshi la muungano wa chama cha Kikurdi wa Syria (PYD). Hata hivyo vyanzo vya kiintelijensia vinasema kuwa wapiganaji hao hawajarejea nyuma na kuvuka Mto Euphrates kama ilivyotarajiwa na Serikali ya Uturuki na Marekani.
Kundi hilo PKK limeorodheshwa kama kundi la kigaidi na Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya. Zaidi ya watu 40,000 wameuwawa tangu waasi wachukue silaha 1984. Alhamis Waziri wa Mambo ya Ndani Efkan alilituhumu kundi hilo kwa kwa kuushambulia msafaria wa kiongozi mkuu wa upinzani Kemal Kilicdaroglu.
Serikali imekuwa ikililaumu kundi hilo kwa mfululizo wa mashambulizi kwa mwezi huu katika maeneo ya kusini/mashariki. Na kundi lenyewe limekiri kuhusika mkasa mmoja wa katika kituo cha polisi.
Jumatano Uturuki ilianzisha mashambalizi makubwa ya ardhini nchini Syria, yakiambatana na zana kama vifauru, vyenye kusaidiwa na mashambulizi ya angani kwa lengo la kuukomboa mji wa Jarablus, operesheni ambayo inahusisha vilevile wapiganaji 1,000 kwa upande wa upinzani.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekwisha sema kuwa operesheni hiyo inawalenga kwa pamoja kundi la Dola la Kiislamu na wapiganaji wa Kikurdi wa kikosi cha YPG.
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Idd Ssessanga