1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msaada kwa Ukraine wagubika maadhimisho miaka 75 ya NATO

5 Aprili 2024

Jumuiya ya Kujihami ya NATO hapo jana Alhamisi ilifanya maadhimisho ya miaka 75 tangu kuundwa kwake kwa ahadi ya kuendelea kuisadia Ukraine kijeshi ili iendelee kupambana dhidi ya vikosi vya Urusi,

https://p.dw.com/p/4eRqc
Brussels | Makao Makuu ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO
Makao Makuu ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO mjini BrusselsPicha: Janine Schmitz/AA/photothek.de/picture alliance

Maadhimisho hayo yalifanyika katika siku ya pili ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi wanachama wa NATO kwenye makao makuu ya jumuiya hiyo mjini Brussels.

Yamefanyika katika wakati jumuiya hiyo inatafakari mpango mpana wa kuipatia Ukraine msaada wa kijeshi unaohitajika kwa kipingi cha muda mrefu bila kusuasua.

Nchi hiyo hivi sasa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa zana vya vita na imeendelea kuyarai mataifa washirika kutuma silaha pamoja na mifumo ziada ya ulinzi wa anga kuisaidia kudungua makombora ya masafa yanayofyetuliwa na Urusi.

Sherehe kubwa zaidi ya kuadhimisha miaka 75 ya kuundwa kwa NATO inatazamiwa kufanyika kati ya Julai 9 na 11 wakati wakuu wa nchi wanachama 32 wa jumuiya hiyo watakapokutana kwa mkutano wa kilele mjini Washington.