1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msalaba Mwekundu: Hali ya kiutu nchini Libya ni mbaya sana

20 Septemba 2023

Shirika la kimataifa la misaada la Msalaba Mwekundu limesema hali ya kiutu katika eneo lililokumbwa na mafuriko mashariki mwa Libya ni ya kutisha kwa wakati huu, watu wengi wakiwa bado hawapati mahitaji muhimu.

https://p.dw.com/p/4WbaP
Inakadiriwa zaidi ya watu 100,000 bado wamefukiwa na vifusi kufuatia janga lililoikumba Libya.
Inakadiriwa zaidi ya watu 100,000 bado wamefukiwa na vifusi kufuatia janga lililoikumba Libya.Picha: IHH/AP/picture alliance

Msemaji wa shirika hilo katika eneo la Mashariki ya Karibu na Kati, Imene Trabelsi amesema waathirika wa mafuriko ya wiki iliyopita wanakosa makazi sahihi, majisafi, umeme na huduma za mawasiliano.

Afisa huyo aidha amezungumzia ugumu wa kuwasiliana na timu zao zilizopo nchini Libya kutokana na changamoto za mitandao ya mawasiliano ya simu na intaneti.

Amegusia pia umuhimu wa kufukua miili ya wahanga wa mafuriko hayo waliofukiwa na vifusi wakati uwezekano wa kuwapata wakiwa hai ukizidi kufifia. Inakadiriwa zaidi ya watu 100,000 bado wamefukiwa na vifusi.