MSF: Ugonjwa wa kipindupindu unaenea 'kwa kasi' Sudan Kusini
6 Desemba 2024Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF limesema katika taarifa kuwa, wagonjwa 737 wa kipindupindu wameripotiwa katika jimbo la Upper Nile ndani ya muda wa mwezi mmoja.
Mlipuko wa ugonjwa huo umeripotiwa zaidi katika mji wa Malakal, lakini umeenea pia hadi maeneo mengine ya nchi ukiwemo mji mkuu wa Juba.
MSF yaeleza wasiwasi kuhusu hali nchini Sudan Kusini
Mji wa Malakal umepokea idadi kubwa ya raia wa Sudan Kusini waliorejea nchini humo kufuatia mgogoro katika nchi jirani ya Sudan, na umeorodesha wagonjwa 37,000 wa Kipindupindu kwa mujibu wa MSF.
Mkuu wa ujumbe wa shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF nchini Sudan Kusini Zakaria Mwatia amesema hali ni mbaya katika mji wa Malakal na kuna wasiwasi juu ya kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo jirani.