1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IS wataandamwa

13 Januari 2016

Msiba kufuatia shambulio la kigaidi la Istanbul, Uturuki: wahanga wasiopungua 8 wa shambulio hilo ni watalii kutoka majimbo 4 ya Ujerumani ; Hessen,Berlin,Brandenburg na Rheinland Pfalz..De Maiziere ziarani Istanbul

https://p.dw.com/p/1HcLA
Mashada ya mauwa kuwakumbuka wahanga wa mashambulio ya IstanbulPicha: Reuters/Y. Karahan

"Waziri de Maizière atafika kule kule ambako shambulio hilo limetokea ambako atazungumza na waziri mwenzake wa Uturuki kabla ya kukutana baadae na waandishi habari.

Wajerumani wasiopungua wanane ni miongoni mwa wahanga 10 wa shambulio la kigaidi la jana asubuhi katika mtaa mashuhuri wa Sultanahmet unakokutikana Msikiti wa buluu na kanisa kuu la Hagia Sofia. Majeruhi tisa kati ya 15 ni wajerumani pia. Aliyefanya shambulio hilo inasemekana ni kijana wa miaka 27 raia wa Syria mwenye asili ya Saud Arabia . Alijiripua kati kati ya kundi la watalii wa kijerumani katika eneo hilo ambalo ni kivutio cha watalii mjini Istanbul. Gazeti la Al Hayat limeinukuu wizara ya mambo ya ndani ya Saud Arabia ikisema familia ya Nabil Fadli waliondoka Saud Arabia kijana huyo alipokuwa na umri wa miaka minane.

Serikali ya Uturuki inawatwika jukumu la shambulio hilo wanamgambo wa dola la kiislam-IS.

Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti kuhusu kukamatwa wanajihadi watatu wa IS. Wote watatu ni raia wa Urusi. Wamekamtwa katika mji wa bahari wa Antalya-Shirika la habari la Dogan halikusema lakini kama wanahusishwa na shambulio la Istanbul au la. Katika msako uliopelekea kukamatwa magaidi hao,nyaraka kadhaa ikiwa ni pamoja na CD zimegunduliwa. Watuhumiwa 65 wa kigaidi wamekamatwa jana pia katika miji kadhaa ya Uturuki.

Huzuni na Msiba nchini Ujerumani

Meya wa jiji la Berlin na wanasiasa wengineo kutoka majimbo ambayo wahanga wa mashambulio ya Istanbul wanatokea wameelezea masikito yao na kutuma rambi rambi kwa familia."Leo ni siku ya huzuni . Tumepania kukabiliana na hatari inayotokana na ugaidi wa kimataifa" amesema meya wa jiji la Berlin Michael Müller kutoka chama cha Social Democratic.

Türkei Polizeiaktion gegen Terrorverdächtige in Izmir
Polisi wawasaka watuhumiwa katika mji wa IzmirPicha: picture-alliance/AA/C. Oksuz

Hakuna bado aliyedai kuhusaika na shambulio la Istanbul,lakini wafuasi wa itikadi kali ya dini ya Kiislam,wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kushoto na wakurd wanaopigana na serikali ya uturuki kusini mashariki ya nchi hiyo,wameshawahi siku za nyuma kufanya mashambulio kama hayo ya kigaidi.Uturuki na

Ujerumanai zapania kuwaandama Magaidi

Waziri mkuu wa Uturuki Ahmed Davotoglu amesema amezungumza na kansela Angela Merkel kutoa rambi rambi za serikali yake na kuahidi Uturuki itaendelea kupambana na IS nyumbani na kupitia ushirika wa kimataifa unaoongozwa na Marekani.

Berlin Merkel zu Terroranschlag in Istanbul
Kansela Sngela Merkel akizungumzia yaliyojiri IstanabulPicha: picture-alliance/dpa/S. Stache

Mwanmdishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AFP/dpa/

Mhariri:Iddi Ssessanga