1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO kubadili msimamo kama Urusi itatumia silaha za nyuklia?

16 Machi 2022

Hakuna mtu anayejua Urusi iko karibu kiasi gani kutumia silaha za kemikali au nyuklia katika mashambulizi yake Ukraine, mashambulizi ambayo yanaweza kuivuruga mipaka. Msimamo wa NATO kuhusu usalama unaweza kubadilika?

https://p.dw.com/p/48Y4D
Bundeswehrsoldaten in Litauen
Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov anataka uchunguzi wa kimataifa kuhusu madai ya serikali yake kwamba Ukraine inatengeneza silaha za kemikali. Sio jambo lisilotarajiwa. Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg siku ya Jumanne alitumia lugha kali katika mkutano na waandishi habari katika kushughulikia kile alichokiita "madai ya kipuuzi" ya Urusi.

Soma zaidi: Msaada wa NATO na Magharibi kwa Ukraine hautoshi

Stoltenberg alisema wameiona Urusi inaishutumu Ukraine na pia washirika wa NATO kwa kutengeneza silaha za kemikali na huo ni uongo mtupu. "Hali hiyo imetufanya tuwe na wasiwasi kidogo juu ya uwezekano kwamba Urusi inapanga kufanya hivyo," alifafanua Stoltenberg.

Siku ya Jumapili Stoltenberg aliliambia gazeti la Ujerumani, Welt am Sonntag kwamba mashambulizi ya kutumia silaha za kemikali itakuwa "uhalifu wa kivita."

Belgien Brüssel | Treffen NATO Verteidigungsminister | Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg Picha: Johanna Geron/REUTERS

Je hilo linatosha kuishawishi NATO kuingilia kati? Rais wa Poland, Andrzej Duda ameizungumzia changamoto hiyo waziwazi. Machi 13, Duda aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC kwamba iwapo Rais wa Urusi, Vladmir Putin atatumia silaha zozote za maangamizi makubwa, basi kutakuwa na haja ya kubadilika.

Duda anasema kwa uhakika NATO na viongozi wake wakiongozwa na Marekani, watalazimika kukaa chini na kufikiria kwa umakini nini cha kufanya kwa sababu itaanza kuwa hatari.

Alipoulizwa na DW siku ya Jumanne iwapo hatua kama hiyo inaweza kuubadilisha msimamo wa NATO, Stoltenberg alisema rais wa Marekani na washirika wengine pia wameweka wazi kwamba iwapo Urusi itatumia silaha za kemikali, itawajibika kwa kiasi kikubwa.

Hofu ya nyuklia

Mbali na matumizi ya silaha za kemikali, hofu inaongezeka kwamba Urusi inaweza kutumia silaha za nyuklia au kusababisha ajali ya miale ya nyuklia katika mojawapo ya vinu vinne vya kutengeneza nishati ya nyuklia nchini Ukraine, kikiwemo kinu kikubwa kabisa barani Ulaya cha Zaporizhzhia, ambacho kilikuwa eneo la mapambano mwanzoni mwa uvamizi wa Urusi.

Siku ya Jumatatu, kampuni ya nishati ya nyuklia ya Ukraine, Energoatom ilitangaza kuwa vikosi vya Urusi vimechukua hatari kama hiyo, kwa kufyatua risasi katika kinu cha nyuklia. Kiwango cha juu cha kutokuwa na uhakika na hali tete kilisababisha kundi la wataalamu wa kimataifa na watunga sera wa zamani, akiwemo aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Igor Ivanov, kutoa taarifa ya pamoja na kuonya kuhusu uwezekano wa matokeo mabaya.

Ukraine-Krieg | Atomkraftwerk Zaporizhzhia angegriffen
Jengo la utawala katika kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia, Ukraine likiwa limeshambuliwa na vikosi vya UrusiPicha: via REUTERS

Huku kila kiongozi wa Dunia anayezungumza na Rais Putin akiwa amehitimisha kwamba kiongozi huyo wa Urusi hana mpango wa kusitisha vita, swali linabaki kuhusu jinsi NATO itakavyojibu kitisho kinachoongezeka cha matumizi ya silaha ambazo zinaweza kuangamiza ndani na nje ya Ukraine.

Sera ya NATO ya kutokwenda

Ian Bond, mkurugenzi wa sera za kigeni katika Kituo cha Mageuzi ya Ulaya, ameiambia DW kwa kuzingatia maneno ya Stoltenberg, kuna uwezekano kuwa Warusi wanafanya mambo ambayo yanaoonesha kuwa wanajiandaa kuanzisha aina hiyo ya mashambulizi.

Veronika Vichova, Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Maadili cha Ulaya kuhusu Sera ya Usalama chenye makao yake mjini Prague, ameiambia DW kuwa hakubaliani na mkakati huo, sio utekelezaji wake, bali mawasiliano yake. Anasema anaamini kuwa NATO inapaswa kukiri wazi kwamba kuna uwezekano wa kutumia silaha zozote za maangamizi makubwa, WMD sio tu kwa Ukraine, lakini kwa washirika wake pia.

Vichova anafafanua kuwa hofu yake kubwa ni ari ya wananchi wa Ukraine ambao wanauawa kila siku wakiitetea nchi yao na ujumbe kutoka NATO, ambao kimsingi unawategemea tu kuendelea na vita. Anasema wanapaswa kutuma ujumbe kuwaambia hatutafanya chochote kuwasaidia.

(DW https://bit.ly/3idfCPm)