1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mtawala wa kijeshi wa Myanmar asema uchaguzi sharti ufanywe

1 Februari 2023

Kiongozi wa kijeshi anayeiongoza Myanmar, Min Aung Hlang, amesema jeshi la nchi hiyo litalinda katiba na kwamba uchaguzi wa vyama vingi sharti ufanyike.

https://p.dw.com/p/4Mym8
Thailand | Protest zum Jahrestag Militärputsch in Myanmar
Picha: Athit Perawongmetha/REUTERS

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali nchini humo, MRTV, jenerali huyo wa kijeshi ambaye hakutoa tarehe ya uchaguzi huo, ametoa wito kwa vikosi vya ulinzi na Baraza la Usalama kurefusha muda wa hali ya hatari kwa muda wa miezi mingine sita. 

Hali hiyo imekuwepo tangu mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwaka 2021

Mitaa imesalia kuwa mitupu na maduka kufungwa nchini humo leo kama sehemu ya maandamano, mnamo wakati nchi hiyo inafanya kumbukumbu ya miaka miwili tangu mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa kiongozi wa kiraia, Aung San Suu Kyi, na serikali yake madarakani.

Myanmar imekuwa katika hali ya machafuko tangu mapinduzi hayo yaliyofuatiwa na ukandamizaji dhidi ya waandamanaji na kuchochea mapigano kote nchini humo na kudhoofisha uchumi.