1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiItaly

Mtoto wa miaka 11 aokolewa baada ya siku 3 baharini

11 Desemba 2024

Mtoto anusuriwa baada ya kukaa baharini kwa siku tatu katika kisiwa cha Lampedusa cha Italia.

https://p.dw.com/p/4o1IH
Mtoto aokolewa baada ya kukaa baharini kwa siku tatu Lampedusa, Italia
Mtoto aokolewa baada ya kukaa baharini kwa siku tatu Lampedusa, ItaliaPicha: Cecilia Fabiano/ZUMA Press/picture alliance/AP

Mtoto wa kike wa  miaka 11 kutoka Sierreleone, aliyenusurika peke yake katika ajali ya boti aliokolewa usiku wa kuamkia Jumatano baada ya kukaa kwa siku tatu baharini katika kisiwa cha Italia cha Lampedusa.

Shirika la hisani la uokozi la Kijerumani limesema wafanyakazi wake wa melini waliokuwa njiani kuelekea kwenye tukio jingine la dharura, walisikia sauti baharini ya mtoto huyo majira ya saa tisa alfariji.

Aliokolewa akiwa amevalia jaketi maalum la kumsadia kutozama huku akiwa anaelea baharini akiwa juu ya boya la kuogelea.

Mtoto huyo aliwaeleza shirika la uokoaji la kijerumani kwamba alisafiri kutoka  mji wa Sfax Tunisia kwa boti ya kuundaunda akiwa na watu wengine 45 na ilizama kutokana na dhuruba ya baharini.