MUMBAI:Waziri Mkuu Manmohan Singh wa India asema India bado imara
13 Julai 2006Matangazo
Waziri mkuu wa India bwana Manmohan Singh amesema hakuna atakaeweza kuifanya India isalimu amri. Waziri Mkuu Manmohan amesisitiza hayo siku moja baada ya kufanyika mashambulio ya kigaidi katika mji wa Mumbai ambapo watu zaidi ya mia mbili waliuawa.
Watu wengine zaidi ya mia nne walijeruhiwa katika mashambulio hayo yaliyofanyika kwenye treni.
Bwana Singh amesema ,hakuna mtu atakaeweza kuziba njia ya maendeleo inayofuatwa na India.
Hadi sasa hakuna habari zozote juu ya magaidi waliofanya mashambulio ya Mumbai.
Hapo awali kulikuwa na tuhuma juu ya kuhusika kwa makundi ya kiislamu yanayopigania uhuru wa Kashmir.