Museveni aongoza katika matokeo ya muda
19 Februari 2011Matangazo
Kulingana na Tume ya Uchaguzi ya Uganda,Rais Museveni anaongoza na mpinzani wake mkuu amepata asilimia 22.9 ya kura zilizohesabiwa mpaka sasa.
Hata hivyo tume hiyo haijatoa idadi kamili ya watu waliopiga kura ila inaaminika kuwa imeipita asilimia 69 iliyokuwako katika uchaguzi wa rais uliopita wa mwaka 2006.Matokeo kamili yatatangazwa rasmi hapo kesho.