1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museveni mshindi tena Uganda

20 Februari 2011

Katika kile kilichotarajiwa na wengi, Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa mara nyengine tena wa uchaguzi akiwapita wapinzani wake kwa mbali, huku upinzani ukikataa matokeo.

https://p.dw.com/p/10Kpq
Rais Yoweri Museveni
Rais Yoweri MuseveniPicha: DW/Schlindwein

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda, imemtangaza rasmi Rais Yoweri Kaguta Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Ijumaa iliyopita (18 Februari 2011), nchini humo.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Badru Kiggundu, amesema kwamba Museveni amepata asimilia 68 ya kura dhidi ya mshindani wake wa karibu, Kizza Besigye, aliyepata asilimia 26.

Hata hivyo, Besigye ambaye amegombea nafasi hiyo kwa mara ya tatu sasa, amekataa kuyatambua matokeo hayo, akiapa kwamba, muungano wa vyama vya upinzani aliouwakilisha katika kinyang'anyiro hiki, utakwenda mahakamani kuyapinga.

Hii ni mara ya nne kwa Rais Museveni kutangazwa mshindi wa uchaguzi, jambo linalomfanya kuwa miongoni mwa marais wa Afrika waliokaa muda mrefu madarakani. Hadi sasa