1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muswada wa Sunak wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda wapita

18 Januari 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak hapo jana aliwashinda wabunge wa chama chake cha Kihafidhina wanaompinga kutokana na mpango wake wa kutaka kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda.

https://p.dw.com/p/4bPXt
Uingereza| Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak Picha: James Manning/AP/picture alliance

Ushindi huo wa Sunak unadhoofisha mamlaka yake na kuzidisha migawanyiko katika chama chake.

Sunak alikabiliana na upinzani kutoka kwa wabunge wanaoegemea mrengo wa kulia katika chama chake waliokuwa wanataka achukue hatua kali zaidi katika muswada wa kukabiliana na uhamiaji haramu, katika hatua ambayo wabunge wenye misimamo ya kati wanahofia kwamba itakuwa inakiuka ulinzi wa haki za binadamu.

Waziri Mkuu wa Uingereza asema yuko tayari kuimarisha mpango wake wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda

Mwisho wa siku, ni wabunge 11 kati ya 60 waliokuwa wanampinga walioamua kupiga kura dhidi ya muswada huo.

Baadhi walihofia kuanguka kwa serikali iwapo hawangeuunga mkono muswada huo.