Mvua kubwa Sudan zasababisha vifo vya watu wasiopungua 68
13 Agosti 2024Matangazo
Karibu watu 68 wamefariki dunia kutokana na mvua kubwa iliyonyesha nchini Sudanmwaka huu. Haya yamesemwa na wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo inayodai kuwa makaazi ya watu yalibomolewa na mitaa kufurika na kuiongezea masaibu zaidi nchi hiyo iliyozongwa na vita.
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOMx, linasema tangu Juni mosi, zaidi ya watu 44,000 kote nchini humo wameachwa bila makao kutokana na mvua hizo. Mvua hizo ambazo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo tangu mwaka 2019, zimeyaathiri maeneo ya magharibi, kaskazini na mashariki mwa nchi hiyo ambapo watu milioni 10.7 wanaishi katika kambi, shule au maeneo yaliyo wazi.