Mwanadiplomasia mkuu wa Iran akamilisha ziara yake UAE
22 Juni 2023Matangazo
Ziara ya Hossen Amir-Abdollahia katika Umoja wa Falme za Kiarabu, inafanyika baada ya kuzuru Qatar, Kuwait na Oman, ikiwa ni hatua ya karibuni zaidi katika msururu wa hatua za kidiplomasia za Tehran inayotaka kupunguza kutengwa, kuboresha uchumi wake na kuimarisha miradi yake.
Mapema leo, viongozi hao walijadiliana kuhusu mahusiano baina ya mataifa yao na namna ya kuimarisha uhsirikiano, hii ikiwa ni kulingana na shirika la habari la WAM la Umoja wa Falme za Kiarabu, wakati mataifa ya Ghuba yakiangazia kupunguza mivutano na Iran iliyochochewa katika miaka ya karibuni na mizozo ya Yemen na Syria.
Kwenye ziara hiyo, Iran ilisaini makubaliano na Umoja wa Falme za Kiarabu ya kutanua huduma usafiri wa anga na kuongeza fursa za biashara na utalii,