1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUfaransa

Mwanaharakati akamatwa kuhusiana na hujuma Olimpiki

29 Julai 2024

Mwanaharakati mmoja anayeegemea kambi ya msimamo mkali wa mrengo wa kushoto nchini Ufaransa amekamatwa leo akihusishwa na tukio la kuhujumiwa kwa miundo mbinu ya reli ya mwendo kasi Ijumaa iliyopita.

https://p.dw.com/p/4irHO
Ufaransa Paris 2024 | Watalii mbele ya ukumbi wa de la Bastille
Watalii wakipiga picha mbele ya pete za Olimpiki kwenye ukumbi wa de la Bastille.Picha: Bernd Kammerer/Presse- und Wirtschaftsdienst/picture alliance

Hayo yametangazwa na waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Gerald Darmanin.

Mwanaharakati huyo ni mtu wa kwanza kukamatwa na kutangazwa hadharani tangu kutokea tukio la kushambuliwa mifumo ya usafiri mjini Paris saa chache kabla ya kuanza kwa sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki Ijumaa.

Soma pia: Ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki Paris 2024

Taarifa zaidi zinasema watu wengine 50 pia wamekamatwa.

Wakati huo huo, gazeti la Le Parisien na kituo cha televisheni cha BFM wametangaza leo Jumatatu kwa kunukuu vyanzo ambavyo havikutajwa, kwamba mifumo ya kampuni ya Telekom inayofungamana na makampuni mawili ya mawasiliano ya Ufaransa imehujumiwa.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW