Nchi kadhaa za Afrika zimesaini mikataba ya biashara inayojulikana kama EPA na Umoja wa Ulaya. Serikali ya Cameroon ina matumaini kwamba mkataba huo utaimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Ulaya. Hata hivyo wazalishaji wa ndani wana hofu kwamba hawatoweza kushindana na bidhaa za Umoja wa Ulaya zitakazoingia nchini humo bila kulipiwa kodi kuanzia Agosti mwaka 2016 na kuendelea.