1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanasiasa wa upinzani 'atekwa nyara' Burundi

13 Septemba 2017

Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Burundi ametekwa nyara katika mji mkuu wa nchi hiyo na watu wenye silaha wakiwa wamevalia sare za jeshi la polisi, kwa mujibu wa familia yake.

https://p.dw.com/p/2juDn
Burundi Präsident Nkurunziza arrives for the celebrations to mark Burundi's 55th anniversary of the independence at the Prince Louis Rwagasore stadium in Bujumbura
Picha: Reuters/E. Ngendakumana

Leopold Habarugira mwenye umri wa miaka 54, ndiye mweka hazina wa chama cha upinzani cha Union for Peace and Development (UPD), na miongoni mwa wanachama wachache wa upinzani waliobakia katika taifa hilo tangu lilipotumbukia katika mgogoro mwaka 2015.

Mke wake wake, Liberates Nzitonda, ameliambia shirika la habari la Ujerumani (dpa) kwamba yeye na mume wake walikuwa wanafanya mazoezi na ghafla wakaona gari linakuja upande wao, likiwa na watu watatu wenye silaha na wakiwa wamevalia sare za polisi, ambao walimchukuwa mume wake na kumlazimisha kuingia kwenye gari lao.

Lakini msemaji wa jeshi la polisi Pierre Nkurikiye, amesema mamlaka hazina taarifa juu ya utekaji huo.