1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bobi Wine kupasuliwa baada ya kupigwa risasi na polisi

4 Septemba 2024

Robert Kyagulanyi Ssentamu almaarufu Bobi Wine alijeruhiwa mguuni na kile kinachodaiwa kuwa risasi na askari polisi nje ya mji wa Kampala, na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

https://p.dw.com/p/4kGGy
Uganda Kampala | Kiongozi wa upinzani Bobi Wine akiwa hospitali baada ya kushambuliwa.
Bobi akiwa hospitali baada ya tukio la kushambuliwa na askari polisi.Picha: Abubaker Lubowa/REUTERS

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine atafanyiwa upasuaji, siku moja baada ya kujeruhiwa mguu katika tukio la vurugu ambapo chama chake jana kiliripoti kwamba alipigwa risasi.

Wakili wa mwanasiasa huyo, George Musisi amefahamisha leo Jumatano kwamba hivi sasa hayuko katika hali mbaya ingawa kwa mujibu wa madaktari atafanyiwa upasuaji kuondowa vipande vya  bomu la kutowa machozi lililompiga mguuni.  

Soma pia: Uganda: Polisi yasitisha mikutano ya siasa ya Bobi Wine

Musisi amesema inaonesha kwenye tukio hilo polisi ililenga kumdhuru mwanasiasa huyo. Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine alipelekwa hospitali ya Nsambya akiwa katika maumivu makali. Jana polisi ya Uganda ilisema itaanzisha uchunguzi juu ya tukio hilo.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW