Serikali ya Libya yamuachia mwanawe Gaddafi kutoka jela
6 Septemba 2021Matangazo
Saad Gaddafi ameachiliwa huru miaka miwili baada ya uamuzi wa kuachiwa kwake kutolewa. Taarifa kutoka kwa serikali inasema Saad aliachiwa na kupelekwa moja kwa moja kwa familia yake.
Serikali imesema imemuachilia huru kama sehemu ya mpango wa kuwaachia wale waliokamatwa kinyume cha sheria. Saad alikimbilia nchi jirani ya Niger baada ya maandamano ya kutaka mageuzi kuanza mwaka 2011.
Babake Moammer Gaddafi alikamatwa na kuuwawa na waasi mwezi Oktoba mwaka uo huo. Mwaka 2014 Niger ilimrejesha Saad nyumbani alikofungwa hadi kuachiwa kwake.
Libya imekumbwa na mgogoro tangu kuondolewa na kuuwawa kwa Gadaffi na imekuwa uwanja wa mapambano kwa makundi hasimu ya waasi.