Mwandishi mahiri wa vitabu vya Kiswahili nchini Kenya na Afrika Mashariki, Profesa Ken Walibora amefariki dunia. Tanzia ya Walibora ambaye aliwahi pia kuwa mtangazaji imejulikana leo asubuhi. Ili kufahamu zaidi kuhusu mazingira yaliyosababisha kifo chake Grace Kabogo amezungumza na Nuhu Bakari, mtaalamu wa lugha ya Kiswahili nchini Kenya ambaye pia ni rafiki wa karibu wa marehemu Walibora.