1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwinyi: Tubadilishe mfumo wa uendeshaji wa mashirika

Salma Said10 Machi 2021

Zanzibar imeamua kurejesha nidhamu ya matumizi ya fedha baada ya mashirika mengi ya serikali kujiingiza na kufunga kiholela mikataba na kusababishia serikali kupata hasara na kutoa mwanya wa wizi na ubadhirifu wa fedha.

https://p.dw.com/p/3qQc7
Sansibar Inauguration Präsident Hussein Ali Mwinyi  Vizepräsident Othman Masoud Othman
Picha: Glenn Carnell/State House Zanzibar

Serikali ya Zanzibar imesema imeamua kurejesha nidhamu ya matumizi ya fedha na utiaji saini wa mikataba baada ya mashirika mengi ya serikali kujiingiza kwenye kufunga kiholela mikataba na kusababishia serikali kupata hasara na kutoa mwanya wa wizi na ubadhirifu mkubwa wa fedha hizo.

Hatua hiyo inafuatia kikao cha Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi na watendaji wa wizara ya fedha na mipango ambapo alibainisha kutoridhika na matumizi pamoja na mikataba inayoingia kati serikali na wawekezaji na washirika wa maendeleo.

“Kuanzia sasa Hazina iwe na kazi ya kutafuta fedha, mikataba iingiwe na sekta husika. Fedha za TASAF, pamoja na fedha nyingi ya mikopo ya wanafunzi zinapotea kutokana na kushindwa kutumia mifumo, mbali na taasisi hizo kupewa fedha”, alisema.

Rais alitaka kubadilika kwa mfumo wa uendeshaji wa mashirika yake huku kutishia kuyafuta mashirika ambayo hayana tija kutokana na kutochangia ruzuku serikalini. 

Rais Mwinyi aonya juu ya ubadhirifu wa fedha

Sansibar | Präsidentschaftskandidat Hussein Mwinyi legt Wahlkomission Formale vor
Rais wa Zanzibar Dk Hussein MwinyiPicha: DW/S. Said

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali akitoa maelezo ya utekelezaji wa maagizo ya Rais, alisema kwa asilimia 90 ya mfumo wa ufuatiliaji na ukusanyaji wa kodi kwa wakati umefanikiwa.

"Wizara imefanikiwa kukamilika kwa asilimia 90 ya mfumo wa ufuatiliaji na ukusanyaji wa kodi kwa wakati, jambo litakalopunguza ukusanyaji wa mapato kwa fedha taslimu na kuondoa utoaji wa risiti za karatasi, mfumo utakaoanza kutumika  April mosi, mwaka 2021."

Katibu Mkuu, Wizara hiyo Dk. Juma Malik Akil kwa upande wake amesema ni wakati sasa wizara hiyo kutuma mapendekezo serikalini kuhusiana na Mashirika ya Serikali yasioleta na tija na kubainisha umuhimu wa kuendelea kuwepo au kuondoshwa.

"Umefika wakati kwa Wizara hiyo kutuma mapendekezo serikalini kuhusiana na Mashirika ya Serikali yasioleta na tija na kubainisha umuhimu wa kuendelea kuwepo au vinginevyo," alisema.

Dk Mwinyi tokea kuiangia madarakani ameanza na kufanya mabadiliko mengi ya kiutendaji ikiwemo kuwawajibisha watendaji ambao amma wanatuhumiwa kwa ubadhifiru au uzembe kazini pamoja na kudhibiti matumizi holela ya fedha huku akihimiza uwajibikaji katika kuwahudumia wananchi sambamba na kuhimiza kudumisha usalama wa nchi na uendelezaji wa umoja wa kitaifa ambao ulirejeshwa na yeye na Maalim Seif Sharif Hamad aliyefariki mwezi uliopita.

 

--