1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Myanmar yaelezea maendeleo yaliyofikiwa kuelekea uchaguzi

19 Desemba 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Myanmar ameuarifu mkutano wa kikanda wa mataifa jirani juu ya maendeleo yaliofikiwa kuelekea uchaguzi wa mwaka ujao katika taifa hilo lililozongwa na machafuko.

https://p.dw.com/p/4oLmQ
Myanmar | Min Aung Hlaing
Mkuu wa baraza la klijeshi Myanmar Min Aung Hlaing akikagua gwaride la heshimaPicha: Aung Shine Oo/AP Photo/picture alliance

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Thailand Maris Sangiampongsa. Sangiampongsa alitoa taarifa kwa waandishi wa habari kwamba kulikuwa na mjadala wa wazi kuhusu hali ya Myanmar uliofanyika huko Bangkok, na kusema waliohudhuria walibaini kuwa mkutano huo una umuhimu kwa vile mataifa jirani yanaelewa hali ilivyo vizuri zaidi.

Akinukuu taarifa ya mwenziwe wa mambo ya nje wa Myanmar, Maris alisema utawala wa kijeshi wa taifa hilo uko tayari kwa mazungumzo yatakayojumiisha pande zote zenye nia ya kufanikisha amani ya taifa hilo.