1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Myanmar yamfukuza balozi wa Timor ya Mashariki

27 Agosti 2023

Utawala wa kijeshi wa Myanmar umemfukuza balozi wa Timor ya Mashariki, baada ya serikali yake kukutana na serikali kivuli iliyozuiwa nchini humo. Utawala huo umeitaja serikali hiyo kivuli kama kundi la kigaidi.

https://p.dw.com/p/4VcgN
Kiongozi wa Myanmar Min Aung Hlaing
Kiongozi wa Myanmar Min Aung HlaingPicha: Aung Shine Oo/AP Photo/picture alliance

Serikali hiyo inayoitwa National Unity, NUG inaundwa na wabunge walioko uhamishoni na wanaotaka kuuondoa utawala wa kijeshi madarakani.

Mwezi uliopita rais wa Timor ya Mashariki Jose Ramos-Horta alikutana na waziri wa mambo ya nje wa NUG, Zin Mar Aung katika mji mkuu, Dili.

Mapema leo, wizara ya mambo ya nje ya Myanmar ililaani hatua hiyo iliyooita isiyo ya kuwajibika ya Timor ya Mashariki na kuagiza balozi wake aliyeko mjini Yango kuondoka kabla ya Septemba Mosi.

Timor imelaani hatua huyi, na kuijibu kwa kuzungumzia umuhimu wa kuunga mkono juhudi zote za kurejshwa kwa utawala wa demokrasia nchini Myanmar.