Mzozo wa gesi washika kasi Tanzania
3 Januari 2013Huku mzozo wa gesi ya mkoa wa Mtwara kusafirishwa jijini Dar es Salaam Tanzania ukizidi kufukuta, sasa baadhi ya wachambuzi nchini humo wanaungana na wakaazi hao wakisema kuwa wana madai ya msingi ya kutaka mkoa wa Mtwara moja kati ya mikoa maskini nchini humo kufaidika na mapato ya gesi hiyo kabla ya taifa zima kunufaika na rasilimali hiyo.
Awali waziri wa nishati na madini nchini Tanzania, Profesa Sospeter Muhungo, alisema haoni wakaazi hao wakiwa na madai ya uhakika. Muhongo alisema kulingana na katiba ya Tanzania rasilimali zinazopatikana nchini ni kwa manufaa ya Watanzania wote bila ubaguzi kauli inayofanana ile iliyotolewa na rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya hivi karibuni.
Kwa kufahamu zaidi mzozo huo Amina Abubakar amezungumza na Gwandumi Mwakatobe ambaye ni Muandishi wa Habari na pia mchambuzi wa sisa za Tanzania. Kusikiliza mahojiano hayo bonyeza alama ya kusikilizia masikioni hapo chini
Mwandishi Amina Abubakar
Mhariri Josephat Charo