Kuna mzozo usio wa kawaida Kusini Mashariki mwa Ulaya, kati ya Ugiriki na Macedonia, nchi ambayo kwa wakati huu inajulikana kama ''Jamhuri ya Macedonia ya Iliyokuwa Yugoslavia''. Kiini cha mzozo huo ni jina Macedonia, ambalo Wagiriki wanadai ni lao, na wanapinga kutumiwa kwa vyovyote na Jamhuri hiyo jirani kwa upande wa Kaskazini.