Na Oscar inamwendea....
27 Februari 2017Sherehe hizo zilianza vyema kabisa huku kukiwa na kejeli dhidi ya Rais wa Marekani Donald Trump na vichekesho kutoka kwa muongozaji Jimmy Kimmel. Kwa miaka miwili iliyopita wacheza filamu weusi hawajaangaa sana kwenye sherehe hizo lakini awamu hii ya 89 ilipata washindi wawili kati ya wanne weusi walioteuliwa.
Watangazaji Warren Beatty na Faye Dunaway walidaiwa kuchukua bahasha ambayo sio – ile ya mchezafilamu bora wa kike Emma Stone – na kwenda jukwaani kwa ajili ya tuzo ya mwisho.
Wakati walisoma "La La Land” kuwa mshindi, wawakilishi wa PwC waligundua kosa hilo na wakakimbia jukwaani kujaribu kuzuia kutolewa hotuba za ushindi. Muongozaji Jimmy Kimmel alijitokeza na kutangaza kuwa ni filamu ya "Moonlight” ndio iliyoshinda huku akionyesha upande wa ndani ya bahasha.
Hatimaye PricewaterhouseCoopers, kampuni ya uhasibu iliyopewa jukumu la kujumlisha kura za washindi wa Oscar na kuyalinda matokeo hayo hadi yatakapotangazwa, iliomba radhi na kukiri kuwa kulikuwa na mkanganyiko wa bahasha za washindi.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu