Naim Qassem aapa Hizbullah haitaacha mapambano
30 Oktoba 2024Akizungumza kupitia hotuba iliyorikodiwa siku ya Jumatano (Oktoba 30), Naim Qassem alisema baada ya mapigo ya kuumiza kutoka kwa Israel, sasa wameanza kujipanga tena kujaza mapengo yaliyo wazi, kuteuwa viongozi mbadala na kuendelea na kazi ya kuratibu masuala yote ya kundi hilo linaloungwa mkono na Iran.
Kwenye hotuba hiyo iliyosambazwa mchana wa Jumatano, Qassem anasema wapiganaji wake wanapigana kwa ajili ya kulinda mamlaka na uhuru wa Lebanon na kukanusha tuhuma kwamba inatumikia maslahi ya Iran kwenye mapambano yake.
Soma zaidi:Jeshi la Israel layashambulia maeneo ya Hezbollah nchini Lebanon
"Si kweli kwamba tunapigana kwa niaba ya mtu yeyote yule. Iran inatuunga mkono, lakini haifanyi hivyo kwa kutaka chochote kutoka kwetu." Alisema.
Kwa upande mwengine, Qassem aliyetangazwa jana kuchukuwa uongozi wa juu wa Hizbullah kurithi nafasi ya mtangulizi wake, Hassan Nasrallah, alisema wangeliendelea na mapigano kadiri inavyohitajika, hadi pale Israel itakapojiondowa kwenye ardhi inazoikalia na kuacha mauaji yake kwenye Ukanda wa Gaza.
Israel yashambulia mashariki mwa Lebanon
Hotuba ya Qassem ilitolewa katika wakati ambapo mashambulizi ya Israel kwenye mji wa kusini mwa Lebanon, Baalbek, yakiporomosha majengo kadhaa, masaa machache baada ya wakaazi wa huko kutakiwa kuondoka.
Meya wa mji huo, Mustafa al-Shall, alithibitisha mashambulizi hayo dhidi ya Baalbek naaaa viunga vyake.
Soma zaidi:
"Ndege za kivHezbollah yamtangaza Naim Qassem kuwa kiongozi mpyaita za adui zimefanya mkururo wa mashambulizi kwenye eneo la Asira katika mji wa Baalbek na mji mmoja wa karibu." Alisema meya huyo.
Mapema asubuhi ya Jumatano, wakaazi wa Baalbek waliyakimbia majumba yao baada ya jeshi la Israel kuamuru mji huo mkubwa kabisa mashariki mwa Lebanon na viunga vyake kuhamwa kwa madai a kuwapa nafasi ya kuwashambulia wapiganaji wa Hizbullah.
Jumla ya watu 1,754 wameshauwa tangu tarehe 23 Septemba pale Israel ilipoanza mashambulizi yake ya wazi dhidi ya Lebabon, kwa mujibu wa rikodi ya wizara ya afya iliyonukuliwa na shirika la habari la AFP, lakini huenda idadi kamili ikawa kubwa zaidi ya hapo.
Marekani yawasilisha pendekezo la kusitisha vita
Hayo yanajiri wakati Marekani na wapatanishi wengine wakiharakisha juhudi za kusitisha vita ndani ya Lebanon na kwenye Ukanda wa Gaza.
Maafisa wa ngazi za juu wa Ikulu ya Marekani wanatarajiwa kuwasili nchini Israel kesho kwa ajili ya mazungumzo hayo ya usitishaji mapigano na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas.
Soma zaidi: Israel yadai kuyashambulia maeneo zaidi ya 100 ya Hizbullah
Pendekezo linalozungumziwa sasa ni lile la usitishaji mapigano kwa wiki mbili, ambapo ndani yake Israel itajiondowa kwenye ardhi ya Lebanon kwa Hizbullah nayo kujiondowa kwenye eneo la kusini mwa nchi hiyo.