Netumbo Nandi-Ndaitwah ameandika historia kwa kuwa rais wa kwanza mwanamke wa Namibia. Akiwa na taaluma ya kisiasa iliyoanza tangu alipokuwa kijana, Nandi-Ndaitwah amewashinda wapinzani wake wa kiume, ikionyesha dalili ya mabadiliko yanayoweza kuondoa mifumo dume nchini humo.