1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Spika wa Zamani, Nancy Pelosi amelazwa nchini Ujerumani

14 Desemba 2024

Spika wa zamani wa bunge la Marekani, Nancy Pelosi amelazwa hospitali ya Landstuhl karibu na kambi ya kijeshi ya kikosi cha anga ya Ramstein Ujerumani wakati akiwa katika shughuli zake Luxembourg.

https://p.dw.com/p/4o9W8
USA, Chicago | Parteitag der Demokraten | Nancy Pelosi
Nancy Pelosi akizungumza jukwaani wakati wa siku ya tatu ya Kongamano la Kitaifa la Kidemokrasia Agosti 21, 2024 huko Chicago,Picha: Andrew Harnik/Getty Images

Kwa mujibu wa msemaji wake, Ian Krager ni kwamba Pelosi, mwenye umri wa miaka 84, alikuwa Ulaya kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 80 ya kile kinachofahamika kama Vita vya Bulge katika Vita vya Dunia vya  II.  Taarifa ya msemaji huyo unasema kwa sasa spika huyo wa zamani yupo chini ya uangalizi wa madaktari na kwamba hatweza kuhudhuria sehemu ya matukio yaliosalia katika ziara yake hiyo. Hakuelezea hali ya jeraha lake au kutoa nyongeza yoyote ya maelezo, lakini mtu anayefahamu tukio hilo alisema kuwa Pelosi alijikwaa na kuanguka akiwa kwenye hafla na washiriki wengine.