1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO inalaani "shughuli mbaya" za Urusi kwenye eneo lake

3 Mei 2024

Mataifa wanachama wa Jumuiya ya Kujihami NATO yameonesha wasiwasi kuhusu mashambulizi yanayohusishwa na Urusi ambayo yanatajwa kuathiri Jamhuri ya Czech, Estonia, Ujerumani, Latvia, Lithuania, Poland, na Uingereza.

https://p.dw.com/p/4fS9T
Ukraine | PK Zelenskyj na Stoltenberg huko Kyiv
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akizungumza wakati wa mkutano wake wa pamoja na waandishi wa habariPicha: Efrem Lukatsky/AP Photo/picture alliance

Taarifa ya jumuiya hiyo inasema matukio hayo ni sehemu ya kuongezeka kwa vitendo vibaya  vya Urusi katika eneo la mataifa washirika wa muungano huo.

Katika majuma ya hivi karibuni asasi yenye dhima na huduma za usalama barani Ulaya ilifichua mfululizo wa shughuli walizoziita ujasusi wa Urusi wa kimtandao na kusababisha mataifa mengine kafanya juhudi za kujihami.

Hata hivyo wanachama wa NATO wameahidi "kuendelea kuimarisha" umadhubuti waodhidiya mashambulizi hayo na kutumia zana zao kwa kukabiliana na kushindana na vitendo hivyo vinavyodaiwa kufanywa na Urusi.