1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO: Tunaendelea kuiunga mkono Ukraine dhidi ya Urusi

11 Oktoba 2023

Marekani na wanachama kadhaa wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO leo mjini Brussels, wameahidi kuendelea kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake na Urusi.

https://p.dw.com/p/4XQ2c
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Virginia Mayo/AP Photo/picture alliance

Katika mkutano wa Kundi la Ulinzi wa Ukraine linaloongozwa na Marekani, waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin ametangaza msaada mpya wa kijeshi wa dola milioni 200 kwa Ukraine na kuongeza jumla ya msaada wa Marekani kwa taifa hilo kufikia dola bilioni 43.9.

Austin ametangaza haya wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, akisema msaada huo unajumuisha mifumo ya kujilinda angani, makombora ya masafa marefu na maroketi na vifaa vya kuzuia mashambulizi ya droni ya Urusi.

Soma pia:Zelensky awaomba washirika kuipatia Kyiv silaha nzito kuelekea msimu wa majira ya baridi.

Haya yanafanyika wakati ambapo vita kati ya Israel na Hamas na ati ati ya kisiasa iliyoko nchini Marekani, vikiwa vinatilia shaka mustakabali wa msaada muhimu wa kijeshi kwa Ukraine.