NATO yaonya kauli za kuvuruga umoja wake
12 Februari 2024Matangazo
Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami NATO Jens Stoltenberg jana Jumapili ametoa onyo dhidi ya mazungumzo ambayo "yanadhoofisha usalama" baada ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kutishia kuhimiza Urusi kushambulia wanachama wa NATO ambao hawajalipa kikamilifu mchango wao kwa jumuiya hiyo.Katika taarifa yake, Stoltenberg amenukuliwa akisema mapendekezo yoyote kwamba washirika hawatalindana yanadhoofisha usalama wao wote, pamoja na ule wa Marekani. Rais huyo wa zamani wa Marekani mara kadhaaamekuwa akikosoa washirika NATO kwa kutoshiriki vyema michango ya operesheni za jumuiya hiyo.