NATO yathibitisha kisa cha mtandao kulenga tovuti zao
13 Februari 2023Matangazo
Afisa mmoja wa NATO ameliambia shirika la habari la Ujerumani DPA, kwamba wataalamu wa jumuiya hiyo wa masuala ya mitandao wanalishughulikia tukio hilo linaloathiri baadhi ya tovuti.
Kauli hiyo imejiri baada ya ripoti za mitandao ya kijamii kudokeza kwamba huenda wadukuzi wenye mafungamano na Urusi wamedukua tovuti ya makao makuu ya operesheni spesheli za NATO (NSHQ).
Kundi la udukuzi la Urusi Killnet, lilidaiwa kuhusika na shambulizi hilo la mitandao. Kundi hilo limewahi kuhusishwa na visa vingine vya udukuzi, ikiwemo Ujerumani kwa kulenga tovuti za bunge, polisi na miundombinu muhimu.