SiasaUrusi
Navalny anaugua maradhi yasiyojulikana jela
13 Aprili 2023Matangazo
Yarmysh anasema Navalny ambaye yuko gerezani amepunguza kilo nane katika kipindi cha zaidi ya wiki mbili tu. Msemaji huyo ameongeza kwamba Navalny amewekwa katika seli ambapo anapokea adhabu huku akiwa na maumivu makali bila kupata msaada wowote wa kimatibabu.
Mwaka 2020, Navalny aliponea shambulizi la sumu wakati alipokuwa safarini kuelekea Siberia ambapo uchunguzi wa maabara ulionyesha kwamba alikuwa amelishwa sumu. Urusi inakanusha kwamba serikali ilijaribu kumuua.
Alitibiwa kwa sumu hiyo nchini Ujerumani ila akarudi Urusi kwa hiari na akatiwa nguvuni mara tu alipowasili na kufungwa jela kwa kesi ya ufisadi ambayo anasema ilichochewa kisiasa.