Nchi za EU zakubaliana kuiwekea Urusi vikwazo vipya
20 Juni 2024Matangazo
Hayo yameelezwa na Ubelgiji ambayo ni rais zamu wa Umoja wa Ulaya. Tangu Urusi ianzishe vita kamili nchini Ukraine, Umoja wa Ulaya umeweka vikwazo kulenga uchumi, taasisi na maafisa wa Urusi. Hata hivyo, Urusi imejitahidi kutafuta njia ya kuvikwepa vikwazo hivyo ili kuweza kuendesha uchumi na shughuli zake za kijeshi.
Soma pia: Putin: Urusi inasalia kuwa mshirika mkubwa wa kibiashara duniani licha ya vikwazo
Lengo la hatua zinazochukuliwa na Umoja wa Ulaya ni kuizuia Urusi kupata teknolojia ya nchi za Magharibi, inayoweza kutumiwa kwa madhumuni ya kijeshi.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amekiri kwamba nchi yake ina wasiwasi huenda vikwazo hivyo vikaziathiri kampuni za Ujerumani zinazouza bidhaa nje ya nchi.