1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Nchi za Magharibi zapendekeza msaada wa fedha kwa Tunisia

26 Julai 2023

Nchi za maghabiri zinahofia kusambaratika kiuchumi kwa Tunisia kunaweza kusababisha mawimbi makubwa zaidi ya wakimbizi kuelekea barani Ulaya na kwa ajili hiyo zimetoa pendekezo la msaada wa fedha kwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4UPQ3
Rais wa Tunisia Kais Saied ashiriki katika mkutano wa tathmini ya mabadiliko ya mifumo ya chakula kwenye makao makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa mjini Rome.
Rais wa Tunisia Kais SaiedPicha: APAimages/Imago Images

Matumaini ya kutiwa saini makubaliano yaliyopendekezwa bado yapo mbali. Shirika la fedha la kimataifa IMF limetenga msaada wa dola bilioni 1.9 kwa ajili ya Tunisia. Nchi hiyo ya Afrika Kaskazini inayokabiliwa na mfumuko wa bei pamoja na madeni ilifikia makubaliano ya awali na shirika la IMF juu ya mkopo huo.

Tunisia inatakiwa itekeleze mpango kabambe wa kiuchumi

Hata hivyo Tunisia inatakiwa itekeleze mpango kabambe wa kiuchumi utakaoondoa ruzuku inayotolewa kwa ajili ya kufidia bei ya mafuta ya petroli. Rais Kais Saied amepinga amri kutoka nje ambazo anasema zinaweza kusababisha umaskini mkubwa.