Ndege imeanguka Guinea ya Ikweta
17 Julai 2005Matangazo
Malabo, Guinea ya Ikweta:
Abiria wote na Watumishi wameuawa wakati ndege ya aina ya Antonov ilipoanguka muda mfupi baada ya kuruka katika mji mkuu wa Guinea ya Ikweta, Malabo. Waziri wa Habari ambaye pia ni Msemaji wa serikali wa nchi hiyo, Alfonso Nsue Mokuy, amesema kuwa anawasiliana na Waokoaji walioko karibu na mji wa Baney, umbali wa km 19 kutoka Malabo, ambako ndege hiyo ndiko ilikoangukia jana Jumamosi. Waziri Mokuy, amekanusha ripoti za magazeti ya nchi yake kuwa ndege hiyo ilikuwa na watu 80 wakati ilipoanguka. Ndege iliyopata ajali, ikiwa ni mali ya kampuni ya Equatair ilikuwa ikitoka Malabo na kuelekea Bata. Ingawaje njia ya kuelekea Bata ni juu ya Bahari lakini imeangukia nchi kavu. Watu sita miongoni mwa 55 waliokuwamo ndani ya ndege hiyo walikuwa Watumishi