1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Ndege ya Azerbaijan yaanguka na kuuwa watu 38

26 Desemba 2024

Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa Azerbaijan, Baku kuelekea Grozny, ambao ni mji mkuu wa Jamhuri ya Urusi ya Chechnya.

https://p.dw.com/p/4oZxZ
Kazakhstan Aktau 2024 | Ndege ya shirika la ndege la Azerbaijan ilianguka karibu na uwanja wa ndege
Ndege ya shirika la ndege la Azerbaijan ilianguka karibu na uwanja wa ndegePicha: Isa Tazhenbayev/Xinhua News Agency/IMAGO

Watu 38 wamekufa baada ya ndege ya abiria ya shirika la ndege la Azerbaijan kuanguka magharibi mwa Kazakhstan Jumatano, ikiwa na jumla ya watu 67, wakiwemo abiria 62 na wafanyakazi watano.

Ndege hiyo aina ya Embraer 190, iliyokuwa ikielekea Grozny, Chechnya, kutoka Baku, Azerbaijan, ilitoka nje ya njia yake, kuvuka Bahari ya Caspian, na kuanguka karibu na mji wa Aktau, ambao ni kitovu cha mafuta na gesi.

Soma pia:Ndege ya abiria ya Azerbaijan yaanguka

Rekodi za mifumo ya ufuatiliaji wa safari za ndege zilionyesha ndege hiyo ikitoka nje ya njia yake kabla ya kuanguka. Manusura 29, wakiwemo watoto watatu, wamelazwa hospitalini.

Abiria walikuwa raia wa Azerbaijan 37, Kazakhstan sita, Kyrgyzstan watatu, na Urusi 16, kwa mujibu wa maafisa wa Kazakhstan.