1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaDjibouti

Ndege ya Baerbock kuelekea Djibouti yaelekezwa Saudi Arabia

25 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema ndege ya nchi yake ililazimika kutua Saudi Arabia bila kupangwa akiwa njiani kuelekea nchini Djibouti baada ya kukosa kibali cha kupaa juu ya anga ya Eritrea

https://p.dw.com/p/4be5n
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock atua katika uwanja wa Jeddah katika ziara kuelekea Djibouti
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani - Annalena BaerbockPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Katika taarifa, Baerbock amesema kutua kwa ndege hiyo nchini Saudi Arabia kulikuwa dhihirisho la ukosefu wa utulivu kwa ujumla katika eneo hilo, kwa sababu anga za nchi za karibu za Sudan na Yemen hazingeweza kutumika kama njia kutokana na migogoro inayoendelea katika maeneo hayo.

Ujerumani na Umoja wa Ulaya kushughulikia usalama katika Bahari ya Shamu

Baerbock ameongeza kuwa alikuwa amepanga kuwasilisha ujumbe nchini Djibouti kwamba Ujerumani na Umoja wa Ulaya zinashughulikia mbinu za kulinda njia za meli katika Bahari ya Shamu dhidi ya mashambulizi ya Wahouthi wa Yemen.

Soma pia:Ujerumani yashinikiza amani Sudan

Djibouti ni kituo cha kwanza cha ziara hiyo ya siku tatu ya Baerbock Afrika Mashariki, ambapo anatarajiwa kufanya mazungumzo kuhusu mgogoro unaoendelea nchini Sudan.

Kenya na Sudan Kusini ni vituo vinavyofuata katika agenda ya Baerbock.