1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yashambulia kituo cha mafuta ndani ya ardhi ya Urusi

14 Desemba 2024

Ndege zisizo na rubani za Ukraine zimekishambulia kituo cha miundombinu ya mafuta katika mkoa wa Orlov wa Urusi na kusababisha moto mkubwa.

https://p.dw.com/p/4o905
Ukraine Angriffe auf Energieversorgung
Mfanyakazi akitazama juu walipokuwa wakirekebisha vifaa kwenye mtambo wa kuzalisha umeme ambao uliharibiwa wakati wa shambulio la kombora, katika eneo lisilojulikana nchini Ukraine Desemba 5, 2024.Picha: ANATOLII STEPANOV/AFP

Taarifa hiyo ya leo ni kwa mujibu wa Gavana wa eneo hilo, Andrei Klychkov. Gavana huyo kupitia ukurasa wake wa telegram hakutoa taarifa zaidi kuhusu eneo lililoshambuliwa lakini ameandika droni 11 zilidunguliwa na kuongeza kuwa hakuna majeruhi. Video ambayo haijaweza kuthibitishwa mara moja iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha moto mkubwa katika kile kinachoonekana kuwa eneo la kiwanda.