1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndugu wa abiria wa MH370 waandamana Beijing

7 Agosti 2015

Jamaa za abiria wa ndege iliyotoweka ya MH370 waliandamana siku ya Ijumaa hadi ubalozi wa Malaysia jijini Beijing huku wengine wakitaka kupelekwa hadi bahari ya Reunion ambapo mabaki ya ndege yanadaiwa kupatikana.

https://p.dw.com/p/1GBYr
MH370 Proteste Familienmitglieder Peking China
Picha: Reuters/J.Lee

Wengi wa abiria waliokuwemo kwenye ndege iliyotoweka walikuwa wachina na karibu jamaa zao thelathini waliandamana karibu na ubalozi huo huku polisi wakifunga barabara. Mapema walikusanyika katika ubalozi huo wakitaka kukutana na maafisa wa ubalozi lakini hakuna aliyejitokeza kuwasikiliza.Wengi walitaka Malaysia iandae safari hadi kisiwa cha Reunion kinachomilikiwa na ufaransa katika bahari ya hindi ambako waziri mkuu wa Maysia alisema ndege hiyo iliangukia.

Madai ya Malaysia kuwa mabaki zaidi ya ndege yake aina ya MH30 iliyopotea yalikuwa katika bahari ya hindi yameishtua Ufaransa huku ikiibua shutma kutoka jamii ya kimataifa kuhusu kupotea kwa ndege hiyo. Tangu kupotea kwa ndege ya Boeing 777 iliyokuwa inatokea jijini Kuala Lumpur kuelekea Beijing mnamo tarehe 8 Mwezi Machi 2014 , maafisa wa Malaysia wamekuwa wakishutumiwa kwa kutoa taarifa zisisizotosheleza na kukataa kutoa maelezo kwa familia zilizoathiriwa na nchi zinazohusika na uchunguzi wa mabaki ya ndege hiyo.

Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak akitoa taarifa mjini Kuala Lumpur, baada ya kupatikana kwa kipande kinachodhaniwa kuwa cha ndege ya MH370 iliyotoweka.
Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak akitoa taarifa mjini Kuala Lumpur, baada ya kupatikana kwa kipande kinachodhaniwa kuwa cha ndege ya MH370 iliyotoweka.Picha: Getty Images/AFP/M. Rasfan

Matumaini yaongezeka

Taarifa ya Waziri mkuu wa Malaysia Najib Rajib Razak siku ya Alhamisi kuwa mabaki yaliyopatikana katika bahari ya Ufaransa yalikuwa ya ndege ya MH70, ilisababisha maafisa wa Marekani, Ufaransa na Australia wanaohusika na uchunguzi wa ndege hiyo kusema kuwa huenda mabaki hayo yakawa ya ndege hiyo.

Waziri wa uchukuzi wa Malaysia LioTiong Lai aliongezea uzito madai hayo kwa kusema kuwa maafisa wa nchi yake wamepata mabaki zaidi katika kisiwa cha Reunion, ikiwemo dirisha na kifaa cha aluminium na kwamba wamekabidhi vifaa hivyo kwa wachunguzi wa Ufaransa kwa upekuzi zaidi. "Ninaweza tu kuthibitisha kuwa ni mabaki ya ndege, siwezi kuthibitisha kuwa ni mabaki ya MH370," alisema waziri Tiong Lai.

Hamu ya Malaysia kuendelea kutoa taarifa inakinzana na ilivyoshughulikia mkasa huo katika siku na majuma ya kwanza ilipojikokota kutoa maelezo muhimu. Mfano ni wakati iliposhindwa kueleza kuwa kifaa cha kunasa safari za ndege cha jeshi ya Malaysia ilinasa ndege isiyojulikana usiku ambapo ndge hiyo ilitoweka.Ingawa serikali ya nchi hiyo ilipata shutma kali ilisimama kidete.

Mwandishi: Bernard Maranga/ape,rtre
Mhariri: Iddi Ssessanga